Home News Business Lifestyle History Entertaiment Sports

fbs forex


fbs forex

JustForex

Saturday, 15 August 2020

Nawezaje kupata Hati za Hakimiliki ya Kimila Tanzania?

UTARATIBU WA KUPATA HATI ZA HAKIMILIKI YA ARDHI KIMILA TANZANIA 

Sheria ya Ardhi ya Vijiji (Sura ya 114) na Kanuni zake za 2001 zimetungwa ili kusimamia Ardhi ya Kijiji. Sheria na Kanuni hizi zimetoa masharti na taratibu mbalimbali zikiwemo za kuandaa na kusajili Hati za Hakimiliki ya Kimila, chini ya fungu la 18-25 l sheria ya ardhi ya kijiji ya mwaka 1999.

SIFA ZA HATI YA HAKI MILIKI YA KIMILA

(i)             Hati ya Hakimilki ya Kimila inatolewa na Halmashauri ya Kijiji kwa raia, kikundi cha raia au chombo kinachotambulika kisheria, chenye wajumbe au wabia ambao ni raia wa Tanzania.

(ii)           Kwa mujibu wa sheria, mila na desturi za raia wa Tanzania, ili mradi sheria na desturi hizo za kimila haziwabagui wanawake, walemavu, watoto au kundi lolote katika jamii ya wanakijiji.

(iii)         Ndani ya Ardhi ya Kijiji.

(iv)          Ndani ya Ardhi ya Hifadhi baada ya mawasiliano na makubaliano na mamlaka ya hifadhi husika.

(v)           Kwa muda usio na kikomo kwa wanakijiji na muda maalumu kwa wasio wanakijiji.

 

Hati ya Hakimiliki ya Kimila ina nguvu sawa na Hatimiliki zinazotolewa na Kamishna wa Ardhi.

Hati ya Hakimilki ya Kimila haitatolewa kwa mtu yeyote, kikundi cha watu, au taasisi ya kijiji isipokuwa au hadi pale ambapo maslahi na mipaka ya ardhi hiyo yatakapokuwa yameamuliwa kama itakavyofafanuliwa katika fungu la 48.

 

Hati miliki tanzania

UTARATIBU WA KUANDAA HATI ZA HAKIMILIKI YA KIMILA KATIKA ARDHI YA KIJIJI.

Hatua zifuatazo zinapaswa kuzingatiwa wakati wa kuandaa Hati ya Hakimiliki ya Kimila

i.      Kutoa Elimu ya Sheria za Ardhi

Elimu itatolewa na Halmashauri ya Wilaya husika katika ngazi ya wilaya na kijiji. Lengo la elimu ni kuelimisha jamii juu ya Sheria na mabadiliko ya utawala na usimamizi wa masuala ya ardhi. 

Sambamba na utoaji wa elimu, Halmashauri itahimiza ujenzi wa Masjala za Ardhi ya Kijiji. Halmashauri ya Wilaya inapaswa kuwa na Masjala ya Ardhi ya Wilaya kwa ajili ya utunzaji wa kumbukumbu na usajili wa Hati za Hakimiliki za Kimila

ii.    Kupima Mipaka ya Vijiji.

Halmashauri ya Wilaya itapima mipaka ya vijiji vyote visivyokuwa na migogoro ya mipaka. Vijiji vilivyopimwa mipaka vitaandaliwa Vyeti vya Ardhi ya Kijiji na kuandikishwa katika Daftari la Vyeti vya Ardhi ya Kijiji la Wilaya.

iii. Kuandaa Mpango Shirikishi wa Matumizi Bora ya Ardhi ya Kijiji.

Vijiji vyote vitaandaliwa Mipango Shirikishi ya Matumizi Bora ya Ardhi kwa lengo la kutenga maeneo kwa matumizi mbalimbali. Mipango itafanywa kwa ushirikishwaji wa Timu ya wataalam ya Wilaya (PLUM), Halmashauri za Vijiji na Timu ya Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ya Kijiji (VLUM). 

Taarifa za mpango, Sheria ndogo na vibao vya kutunza maeneo ni matokeo ya mpango huo.

KUAMUA/KUHAKIKI MASLAHI KATIKA ARDHI.

Uamuzi/Uhakiki wa maslahi katika Ardhi ya Kijiji unaweza kufanyika kwa njia mbili.

i.      Uamuzi/Uhakiki wa Kijiji Kizima/Sehemu ya Ardhi ya Kijiji (Systematic/Village Adjudication)

Timu ya Wilaya ya Usimamizi wa Matumizi ya Ardhi (PLUM) ikishirikiana na Timu ya Uamuzi/Uhakiki Ngazi ya Kijiji itahakiki maslahi kwa mpangilio katika kila kipande cha ardhi na kutoa namba ya Utambulisho wa Kipande cha Ardhi (UKA) kwa kila mmiliki. 

Vipande vyenye migogoro havitahakikiwa mpaka migogoro hiyo itakapotatuliwa na Kamati ya Uamuzi/Uhakiki Ngazi ya Kijiji. Fomu Na. 18 & 50 itajazwa maelezo ya mwombaji, kusainiwa na mwombaji, Mwenyekiti wa Kijiji, Afisa Mtendaji wa Kijiji na Wajumbe wa Kamati ya Uamuzi/Uhakiki Ngazi ya Kijiji. 

Mwombaji atapigwa picha na kumbukumbu zitakazokusanywa zitatumika kuandaa Hati za Hakimiliki ya Kimila.

ii.    Uamuzi/Uhakiki wa Eneo Maalum (Sports Adjudication)

  • Uamuzi/Uhakiki wa Maslahi kwa mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu, utafanywa na Halmashauri ya Kijiji kwa kuteua wajumbe watatu miongoni mwao na majirani wanaopakana na mwombaji. 
  • Mwombaji atajaza Fomu Na. 18 & 44 na kusaini, pia itasainiwa na Mwenyekiti wa Kijiji, Afisa Mtendaji wa Kijiji na Wajumbe watatu wa Halmashauri ya Kijiji waliohusika katika kufanya uamuzi/uhakiki. 
  • Mwombaji atapigwa picha na kumbukumbu zitakazokusanywa zitatumika kuandaa Hati ya Hakimiliki ya Kimila.

Maandalizi, Utoaji na Usajili wa Hati za Hakimiliki ya Kimila. 

  • Wataalam wa Ardhi katika Halmashauri ya Wilaya (Afisa Ardhi na Mrasimu Ramani mwenye taaluma ya GIS) wataandaa nakala tatu (3) za Hati za Hakimiliki ya Kimila.  Maelezo yaliyopo katika fomu Na.  18 & 44 au 18 & 50, picha ya mwombaji na mchoro wa kipande cha ardhi husika vitatumika katika kuandaa hati. 
  • Maandalizi ya hati yatafanywa kwa kutumia karatasi maalum (crested paper).
  • Nakala tatu (3) za hati zilizoandaliwa zitasainiwa na mwombaji, Mwenyekiti wa Kijiji na Afisa Mtendaji wa Kijiji na zitagongwa lakiri/muhuri wa duara wa Halmashauri ya Kijiji na lakiri ya Halmashauri ya Wilaya na kusajiliwa na Afisa Ardhi Mteule.
  •  Baada ya usajili nakala moja ya mmiliki itawekewa karatasi laini (lamination porch).  Mwombaji atalipia kiasi cha fedha kulingana na kitakavyopangw na serikali kwa mwaka huo w fedha.
  • Hati zitakazoandaliwa kwa ajili ya taasisi iliyosajiliwa kisheria, itasainiwa na viongozi wawili wa taasisi hiyo walioteuliwa na kugongwa lakiri ya taasisi husika. 
  • Hati iliyosajiliwa na Afisa Ardhi Mteule inayobaki na kutunzwa katika Masjala ya Ardhi ya Wilaya itagongwa muhuri maalum (counterpart (W) na itakayotunzwa katika Masjala ya Ardhi ya Kijiji itagongwa muhuri maalum (counterpart (V).


Kama umependa makala hii shirikisha na wengine Asante

1 comment:

Forex News