Home News Business Lifestyle History Entertaiment Sports

fbs forex


fbs forex

JustForex

Monday, 24 August 2020

Nawezaje Kufanya Biashara ya Forex Bila Kuwa na Pesa?

forex business

 

Biashara ya Forex Online.

Biashara ya fedha (Forex) ni nin? Hii ni bishara kama biashara nyingine ya bidhaa unaweza kunua mchele mashambani kwa bei kubwa ukaja sokon dar es salaam ukakuta bei imepanda ukauza kwa bei ya juu ukapata faida au unaweza kuta bei imeshuka ukauza bei ya chini ukapata hasara.

Tofauti ya hii na biashara nyingine ni kuwa unaongezewa ulicho nacho ili uwekeze Zaidi na pia bei inapanda na kushuka kwa muda mfupi sana yan ndani ya sekunde.

Kwa nini watanzania wanaogopa biashaa hii? Watu wengi wamekuwa wakitamani kujua na kuweza kufanya biashara ya fedha mtandaoni, lakin wamekuwa wakikosa fursa hiyo ya kujua. Lakin pia kumekuwa na matapeli ambao wanawaambia watu watume hela ili wakusaidia hii sio sahihi. 

Kwa ujumla changamoto ambayo inawakwamisha wengi ni baadhi ya makampuni kuweka kianzio kikubwa hivyo watanzania wengi wakashindwa na hata hivyo hakuna aliye tayari kuwekeza fedha nyingi sehemu moja.

Mambo ya Msingi kwenye Bishara ya Fedha Mtandaoni (Forex)

1.     Kianzio cha Biashara ni kiasi gani?

Biashara ya fedha inasimamiwa na bank za biashara, hivyo kuna Kiwango cha chini ambacho bank kimeweka ili uweze kufanya biashara  ambacho ni unit 100,000 yani kama ni dolla basi $100,000 hii huwa wanaita standard lot, lakini kuna Kiwango kingine kama  min ambayo ni unit 10,000 na macro unit 1,000, nashauri sana uchague macro kwa kuanzia. Hivyo hakuna mfanya biashara wa kawaida atakubali kuweka hela zote hizi, hii ikasababisha kuwepo na mawakala/brokers ambao hawa wanaunganisha wafanya biashara (retail traders) na Banki. 

Mawakala hawa wanatoa kitu kinachoitwa leverage yani ni kama kiasi cha fedha unachoongezewa ili uweze kujiinua na kufanya biashara.Kila Wakala anaruhusu mtu achague leverage anayoitaka hivyo kupitia leverage unaweza kufanya biashara ukapata faida kubwa.

Mfano umechagua leverage ya 1:100 maana yake wewe utahitaji 1% na broker atakupa 99% ili kukuwezesha kufanya biashara. Hivyo ukichagua leverage kubwa ndio unawekewa hela nyingi Zaidi. Hivyo usiwe na wasiwasi unaweza kuwekeza hata $ 1 maana leverage ipo kukusaidia utimize ndoto zako.

Jambo la muhimu kuliko yote wapo baadhi ya mawakala wanatoa demo account kwa ajili ya wanaoanza na ukipata faida basi unaichua wewe.  Kupitia hapa tutakuwezesha kufungua hiyo account ili uanze kukua na kupata faida kubwa Zaidi. Mfano wa kampuni hiyo ni   FBS Forex Market kampuni hii inakupa dolla 100 kama demo na Ukifanya biashara ukapata faida dolla 100 ni za kwako.

2. Napataje Faida kwenye biashara ya fedha?

Ili upate faida maana yake unanunua au unauza jozi ya pesa mfano EURO/USD yani ukinunua maana yake unasubiri bei ipande ufunge upate faida na ukiuza maana yake unasubir bei ishuke ufunge order upate faida. Chukulia umenunua EURO/USD 1.0964 bei ikapanda ukafunga kwa 1.0971 tofauti hapo inakuwa 0.0007 hii ndio faida ni ndogo sana kwa sababu ujatumia  leverage lakini pia faida ya biashara ya fedha inapigwa kwa kutumia pip.

Pips ni nin?

Hii inawakilisha nafasi za desimali za kilichobadilika kwenye jozi ya fedha, kuna baadhi ya fedha zinakuwa na nafasi 2,4 na 5. 

Kwa huo mfano hapo juu maana yake hizo ni pip 7, kama umechagua macro leverage unit 1000 maana yake kila pip ni usd 0.1 kwa mfano hapo juu utapa 0.7 usd kama faida, lakin kama umechagua leverage ya min unit 10,000 utapata faid ya usd 1 kwa kila pip maana yake utapata faida ya USD 7. Na kama ni standard utapa 10$ itakuwa sawa na 70$.

Utaona namna leverage na lot size inavyofanya kazi na kuweza kupata faida. Tutazijadili kwa undani Zaidi kwenye masomo yajayo. Uwepo kwa leverage ndio kumefanya biashara hii ya fedha ikawa na faida kubwa kwa kuwekeza fedha kidogo.

3.     Nifanye biashara ya fedha sehemu gani?

Lakin pia bank hazina mfumo wa kuwezesha wafanya biashara kufanya biashara hii kwa mitandao hivyo broker wametengeneza mfumo.Ipo platform Maarufu inaitwa Meta trade ukijiunga unadownload na bure kabisa inafaa kutumika kwenye computer, simu za android na iphone. Mfumo huu unatumia na broker wote na unakupa fursa ya kuona live mabadiliko ya bei ya soko, faida na hasara.

4.     Muda wa kufanya biashara ni upi?

Katika biashara ya fedha hili ni la muhimu sana, kwa kawaida siku za weeend mfumo unazimwa hakuna biashara. Mfumo unakuwa wazi kuanzia Jumatatu saa 00:00 usiku hadi ijumaa saa 23:59 usiku. Likin pia unapswa ujue muda ambao masoko ya fedha ya baadhi ya nchi yanafunguliwa na kufungwa maana tunatofautiana  masaa, tutakuwa tunatuma muda huo kila siku. 

Muda ambao soko lipo waz hata hali ya bei inachangamka mfano kwa London soko linafunguliwa saa tatu asubuhi na kufungwa saa 11 jioni.

Lingine la msingi ni sikuku za baanzi ya nchi maana siku hiyo pia soko linafungwa kwa nchi usika kwa maana hiyo fedha yao itakuwa inauzika taratibu sana. Inashauriwa kutokufanya biashara ya fedha husika siku hiyo.

5.     Je ni lazima kufunga biashara siku hiyo hiyo?

Mara nyingi biashara ya fedha inatakiwa ukifungua oder ufunge siku hiyo hiyo lakin kama imeshindikana labda kwa kuhofia kufunga biashara yenye hasara ukiwa na matumaini kesho yake bei itakuwa nzuri na upate faida inaruhusiwa. Kama hutashindwa kufunga biashara usiku husika kuna kitu kinaitwa swap rollover hii inatozwa kwa asilimia ya ulichowekeza.

 Hii ni interest rate unajua kwenye biashara ya fedha wew humiliki fedha bali una hodhi (speculate) hivyo ukikaa nazo mpaka kesho kunakuwa na riba (interest rate) amabayo inatozwa na bank. Inweza ikawa faida au hasara kwa kuwa ni tofauti ya interest rate kati fedha mbili ulizohonzi mfano EURO/USD. Broker huwa anaandika kabisa kwa hiyo kama ikiwa chana ni faida kwako ikiwa hasi ni hasara lakin kinakuwa ni kiasi kidogo sana inaweza kuwa 0.01 usd au -0.007.

 

6.     Nitajuwaje kama nikipata hasara kubwa kuliko nilichonacho?

Unaweza ukawa umefungua account kwa broker ukaweka mfano USD 5 halafu ukanunua 1USD ukifikiri bei itapanda badala yake ikashuka sas inavyozidi kushuka usipofunga position hasara inazidi kuongezeka na ikipanda usipofunga position faida inazidi kuongezeka. Sas ikishuka mpaka ikafika kiasi kilichobakia ni 20% au badhi ya broker wameweka 40% watakutumia ujumbe ili uongeze salio kwenye account na ukishindwa basi order ya biashara yako itajifunga yenyewe hii inafanyika ili kuepuka account yako kubakiwa na negative balance.

Kumbuka biashara ya fedha bei inapanda sana na kushuka kwa muda mfupi sana ili kuepuka order yako kufunga Automatic tena kwa hasara nakushauri ukishaona hiyo hali ya hasara inazidi kuongezeka na marginal level au kilichobakia ni 80% fanya kitu kinachoitwa hedging yana unanunua na kuuza kwa wakati mmoja aina moja ya fedha. Tutalezea zaidi kwenye vipindi vijavyo.

 

7.     Je nalazimika kukaa kwenye simu au computer muda wote kuangalia kama bei imebalika na nimepata faida nifunge position?

Unaweza kufanya njia tatu ya kwanza ni kama una muda unaweza kukaa ukawa unaangalia trend ya soko na ukafunga order au kufungua order mpya. Hii nja ni nzuri maana inakufanya kujifunza na kufanya maamuzi manual lakin mbaya sana hasa kwa mtu mwenye mwemko kubwa na kupaniki anajikuta kafanya maamuzi ambayo atayajutia.

Imagine unaona hasara inazidi lakin kumbe baada ya muda unaona soko linabadika unapata faida au unaona kafaida kidogo tu unafurahi unafunga oder kumbe baadae faida ingekuwa kubwa mara mia. Sio lazima kukaa na kuangalia screen muda wote unaweza kuset alert kweye mfumo bei ikifika unayotaka alamu inaita unafunga order manual.

Njia ya pili ni kufanya automatic yani wew unaweka kwamba ikifikia faida kiasi fulani order ifungwe na bei ikifikia sehemu fulan oder mpya ifunguliwe. Pia unaweza ukaweka sehemu kwamba hasara mwisho kiasi gani. Ukishaweka yotehayo kila kitu kitafanyika automatic hata kama huupo kwenye internet ukija jioni unaangalia tu mahesabu yako. Njia ya Tatu ni kutumia Expert Adviser yani kila kitu kinafanyika automatic hii sio nzuri kwa anayeanza.

8.     Je nawezaje kujua hali ya soko?

Ukitaka ufanye biashara ya fedha ufurahi fuatiliaa forex news ambazo zinatolewa. broker unayemchagua mfano FBS Market Inc,  InstaForex,  Huwa wanatoa update ya hali ya uchumi. Hii itakuafanya ujue kama fedha itapanda au itashuka. Pia angalia hali ya fedha husika kwa siku zilizopita ilikuwaje.

Kumbuka hii sio Kamari ni biashara kama biashara nyingine hivyo lazima uwe na taarifa sahihi ili ufanye maamuzi sahishi.

9.     Je nawezaje kufanya biashara bila hasara?

Mfanya biashara yoyote ni risk taker na hakuna biashara isiyo kuwa na faida na hasara lakini zipo njia za kupunguza hatari ya hasara, njia rahisi ni ya kutumia hedging hii unanunua na kuuza kwa wakati mmoja kwenye jozi moja mfano EURO/USD hii itakusaidia kama bei itapanda unapata faida lakin kama itashuka unapata faida. Hakikisha idadi ya unachowekeza kinalingana ili kuepuka maginal level kubadilika mfano unanunua 1 usd unauza 1 usd kwa wakati mmoja. Endapo utatumia njia hii hakikisha unajua ni muda gani wa kuingia sokon na kutoka sokoni. Tutatoa elimu zaidi kwenye maada zijazo.

10Je nawezaje kujua uhalali wa biashara hii? Na malipo yanafanyikaje?

Kama nilivyosema hapo juu kama ukianza na account ya demo maana yake unapewa bonus ya dolla 100 uhitaji kuweka hela. Lkain ukishapata faida kuanzia dolla 100 unaweza kuitoa. 

Kwa Tanzania unaweza kutumia njia ya mastercard yako ya bank au visa kadi pesa yako unaipata muda huo huo kwenye account yako ya bank. Mfano wa kampuni amabazo zimesajiliwa na taasisi ya Fedha Duniani (IFSC) ni FBS Market Inc,  InstaForex,  LITEFOREX na XM FOREX, yapo makampuni mengi lakini mim napendekeza haya maana yanahudumia watu wote Tanzania Ikiwepo yna Kiwango cha chini kianzio, na vigezo vingine nitavitoa kwenye mada zijazo.  

Ikiwa pia umeamua kufungua account ya biashara ukaanza na mtaji wa olla 1 au 5 njia rahisi ya kuweka ni kutumia mastercard au visa card ya bank.

Lakin pia ipo njia nyingine ambayo ni rahisi na nisalama Zaidi ambayo hata mimi naitumia ni kufungua mastercard na mpesa ambayo ni bure kabisa na haraka Zaidi bonyeza *150*00# lipa na mpesa chagua mastercard halafu fuata maelekezo.

Ili kujua kuwa kampuni n halali utaangalia usajili wake kwenye link hapa chini. Epuka kumtumia mtu hela pesa unaweka kwenye account yako uliyofungua kwa broker usika na ni salama kabisa ikiwa umekosea kitu wakati wa kuweka au kutoa pesa basi pesa inarudishwa kwenye account yako.

 

Somo hili ni la utangulizi tutajifunza kipengele kimoja kimoja hadi ufikie hatua ya kufungua account na kuanza kufanya biashara kwa mara ya kwanza.

Ufafanuzi muhimu wa maneno ambayo  kila mfanyabiashara anapaswa kujua ili afanye uchaguzi sahihi kwa kujua

LOTS

Lot ni neno ambalo lipo sana kwenye forex, hii ni idadi ya vipande vya sarafu. Lot moja ni Kiasi  sawa na vipande 100,000 vya sarafu ambyo ni standard / sarafu ya akaunti yako ya kianzio.

 Inamaanisha kwamba ikiwa unataka kufanya biashara ya EUR / USD, utahitaji $ 100,000. Kuna saizi zingine mbili zinazojulikana. Ni mengi kidogo sawa na vipande 10,000 (min unit 10,000) na mengi mengi sawa na vipande 1,000 ( macro unit 1000).

Ili kufungua biashara, utahitaji kuamua ni pesa ngapi za kuweka. Neno 'lot' linahusishwa sana na maneno kama vile 'leverage' na 'pip'. Wacha tuingie kwa undani katika maneno yote.

PIP

PIP inamaanisha "Asilimia katika Uhakika wa decimali". Inawakilisha mabadiliko madogo ambayo jozi ya sarafu inaweza kufanya. Kawaida, jozi huhesabiwa katika nambari nne za decimal, kwa mfano, chukulia sarafu ya GBP / USD hupewa kama hii: 1.3451. lakini, kuna jozi kadhaa ambazo zina pointi 2 za kukadiriwa. Kwa mfano, Dola ya Amerika / yen ya Kijapani imenukuliwa kama 109.70. PIP linawakilishwa na idadi ya mwisho ya bei yani viwango vya decimali.

Mfano Ikiwa EUR / USD ilibadilika kutoka 1.0900 hadi 1.0909, hii itakuwa mabadiliko ya pips 9. Ikiwa USD / JPY ilibadilika kutoka 120.00 hadi 120.11, hii itakuwa mabadiliko ya pips 11. Kwa hiyo mabadiliko yanaweza kuwa chanya au hasi kama ni chanya ni faida na hasi ni hasara.

Kumbuka kuwa madalali wengine wa Forex pia huhesabu viwango 5 na 3 vya desimali na hufanya hesabu kuwa pana na rahisi Zaidi hivyo mtu kupata faida kubwa mfano dalali kama FBS anatumia viwango 5 na 3 vya decimali.

Je pip moja inathamani kiasi gani? yan chukulia ukiipeleka kwenye dolla

Chukulia una macro account ambayo 0.01 lot n sawa na vipande 1000 vya sarafu husika, ikiwa una leverage ya 1:1000 . Ikiwa umenunua Euro/usd kwa 1.9867 ukafunga kwa 1,9868 basi tofauti hapo inakuwa ni 0.0001 hii ni sawa na 1pip kwa viwango vine vya decimal

0.0001$ (1pip) x 1000$ (unit for macro) =0.1$/pip

Hii inategemea umechagua aina gani ya Account kwa standard yenye unit 100,000/ pip moja ni sawa na $10 na mini unit 10,000 ni sawa na $1 kwa pip.

LEVERAGE/KIASI CHA KUKUINUA

Leverage Maanake yake ni Kumpa Uwezo wa Kujiinua humruhusu mfanya biashara kuwa na pesa zaidi kuliko aliyonayo kwenye akaunti yake. Kiasi gani Zaidi huongezwa? Madalali tofauti hutoa ukubwa tofauti wa ukuzaji/leverage. Unaweza kuangalia ukuzaji uliotolewa na FBS  katika kwa kila aina ya account.

Kwa mfano, ikiwa una ukuzaji/leverage wa 1: 100, utahitaji kutoa tu 1% ya ukubwa wa biashara uliotaka na nyingine 99% utaongezewa na broker ili kufanya biashara yako ifanyike. Ikiwa utachagua leverage ya 1:50, utahitaji kutoa 2% ya ukubwa wa biashara (1/50 = 0.02). kwa hiyo wakati wa kufungua account kuna sehemu utajaza leverage unayoitaka, inaruhusiwa kubadilisha baadae lakin ni kwa mara moja tu kwa siku.

Je! Kwanini broker wanawapa wafanyabiashara leverage?

Ukweli ni kwamba ukubwa wa lots/kianzio kwenye Forex ni kubwa sana. Ukubwa wa chini cha msimamo msimamo ni 0.01 lots sawa na unit 1000. Mfano Kwa jozi ya sarafu ya EUR / USD ambayo inachukua euro 1,000. Sio kila mtu atakayetaka kufanya biashara ya pesa atakuwa nazo, haswa mwanzoni. 

Kama sababu hiyo, madalali wanawapa wafanyabiashara fursa ya kuwekeza sehemu ndogo tu ya pesa na wao kufadhili biashara hiyo kupitia leverage. Ni jukumu la kila mtu kuchagua leverage anayotaka kutokana Kiwango alichonacho cha kuwekeza yan ukiwa na hele ndogo utachagua leverage kubwa ili uongezewe nyingi.

Mfano. Unataka kufanya biashara ya lot 0.1 kwa USD / CAD.

Hali 1. Unapaswa kutoa $ 100,000 (1 standard lot) ili uweze  hufanya biashara yako kama haikopi pesa kutoka kwa broker (hakuna leverage).

Hali ya 2. Unaweza kuweka tu $ 100. Katika kesi hii, utahitaji ujumuishaji wa leverage ya 1: 1000. Kwa ufikiaji huu wa Kiwango kinachotakiwa, dalali wako atatoa $ 9,9900 iliyobaki kukusaidia kufungua biashara.

Unaweza kuchagua saizi ya leverage ambayo ungependa kutumia. Ukuaji mkubwa zaidi, faida zaidi utapata kutoka kwa kila order. Wafanyabiashara wenye ujuzi wanaweza kutumia leverage  kubwa ili kupata faida haraka na / au kwa idadi kubwa.

Wakati huo huo, unapaswa kujua kila wakati kuwa hatari zako/hasara pia zinaongezeka kwa ukubwa wa leverage. Ikiwa ulifungua biashara ya ununuzi lakini bei inashuka, kila bei inaenda dhidi yako itakuletea hasara kubwa zaidi ya kile ulichonunua. Unapaswa kuwa mwangalifu na uchague saizi ya kukuza wastani wa leverage. Leverage  kawaida ya kati ya wafanyabiashara wa Forex ni 1: 100.

Margin

Unaweza kuwa unashangaa ni jinsi gani madalali wanaishi kwenye soko ikiwa wanaruhusu wafanyabiashara kukopa pesa nyingi kutoka kwao. Jibu ni kwamba madalali wanalindwa kwa sababu ya magnin Kiwango cha mwisho. Margin ni kiasi cha pesa unachohitaji kuwa nacho kwenye akaunti yako ili kufungua na kudumisha biashara iliyofunguliwa. Yote kwa yote, ikiwa ni utatumia  leverage kubwa zaidi basi magin unayotumia itakuwa  ndogo zaidi ili uweze kufanya biashara.

Katika platform yako ya biashara megatrade 4 unaweza kuona Balance”, “Equity”, “Margin”, and “Free margin”. Kwa hivyo, margin ni kiasi cha pesa tayari umetumia: Jumla hii inafadhili biashara yako iliyowazi sasa. Kiasi cha pesa ambacho unaweza bado kutumia kwa biashara mpya huonyeshwa katika eneo la "free margin".

 

Margin call and Stop Order

Hichi ni kitu cha muhimu sana ambacho wafanya biashara wengi hawakijui hivyo kuishia kupata hasara pasipo kujua. Hta mimi nakiri sikuwa najua hili.

Madalali kawaida hufafanua kiwango cha "margin call" wakin wengine wanficha sana mpaka uwe msomaji ndio utajua. Kiwango hiki kinawakilisha asilimia fulani ya kiasi. 

Ikiwa unayo biashara inayopoteza na usawa wako unaanguka kwa kiwango hicho, utapata onyo kutoka kwa broker kwamba unahitaji kufunga biashara yako au kuweka pesa zaidi kukidhi mahitaji ya kiwango cha chini cha kiasi. Seva ya biashara inaweza pia kufanya uamuzi wa kufunga biashara moja kwa moja kwa kuanza na biashara inayopoteza sana.

Kuna pia kiwango kinachoitwa "stop out". Hii inatokea Ikiwa unaendelea kupoteza pesa kwenye biashara isiyofanikiwa. Ikiwa hasara zako zitavuta usawa wako kwa kiwango cha salio lako, basi broker atastahili kufunga nafasi yako ya biashara bila maonyo yoyote. Hii inasaidia kuepuka kubakiwa na negative balance kwenye account.

Kwa FBS, majin ya kiwango iko kwa 40% na chini. Inamaanisha kwamba utapata magin call ikiwa  akaunti yako itashuka hadi 40% ya ulichowekeza (kwa mfano, 40% ya $ 10 ni $ 4). Stop out/ kusimama ni sawa na 20% kwa FBS, kwa hivyo biashara yako itafungwa moja kwa moja ikiwa usawa wako utashuka hadi $ 20 (20% ya kiasi na chini ya ulichowekeza).

Kila dalali anakuwa na kiwango chake. Majini inahitajika kwa usalama wa dalali na wako ikiwa soko litaenda kinyume na matarajio yako. Ni kwa faida yako kama mfanyabiashara ili kuzuia margin. Ikiwa wewe ni mwangalifu na uzingatia kanuni za usimamizi wa hatari/risk, utaweza kufanya hivyo na kufanya biashara na faida. Tutakuja kuangalia njia ya kuepuka hili.

 

 JINSI MANENO HAPO JUU YANAVYOFANYA KAZI KWA PAMOJA NA UPATE UELEWA

Je ni kiasi gani kinahitajika kuanza biashara hii

Kumbuka kuwa kuna akaunti za demo ambazo hukuuruhusu kufanya biashara bila kuwekeza dola moja. Mfano Saizi ya akaunti ya demo na FBS inaweza kuwa hadi dola milioni moja ila kwa sasa ni dola 100. Akaunti ya demo itakuruhusu kufanya mazoezi ya kuagiza fedha na kuweka ukubwa wa msimamo. FBS inakupa fursa ya Account hii na unaweza kufanya biashara ukapata faida. Kumbuka kuna baadhi ya account za demo wanalipa faida kama FBS.

Ikiwa uko tayari kufanya biashara ukitumia akaunti halisi na upate pesa halisi, unapaswa kujua kuwa kiwango cha pesa unahitaji kuanza biashara inategemea aina ya akaunti unayochagua na dalali unayemtumia. Kwa mfano, ili kufanya biashara kwenye akaunti ndogo utahitaji kuweka angalau $ 5.

 Utaweza kufungua maagizo ambayo kiasi chake huanza kutoka lot 0.01 na utumie leverage nzuri. Pia unaweza kufungua akaunti moja ya kila aina. Ili kuweza kufungua hadi akaunti 10 za aina yoyote.

Hifadhi/Deposit yako huamua ukubwa wako wa biashara

Saizi ya chini ya biashara kwa madali wengi mfano FBS ni lot 0.01. Mengi kidogo (Macro account) ni saizi ya kiwango cha kawaida katika soko la sarafu.Ukichukua vipande 100,000 vya sarafu ya msingi ambyo ndio lot 1, kwa hivyo lot  0.01 hufanya hesabu za vipande 1,000 vya sarafu ya msingi. Ikiwa utanunua lot 0.01 ya EUR / USD na leverage  yako ni 1: 1000, utahitaji $ 1 kama kiwango cha biashara hiyo.

Ikiwa umeweka $ 5 kwenye akaunti ndogo, utaweka amana hii na utaweza kufungua biashara nyingine 4 za saizi hii. Maana yake $4 zinakuwa kama margin na ukipa hasara haitakiwi iwe chin ya assilimia 20% yan $ 1. Ikifikia hapa basi biashara yako itafunga yenyewe kuepuka kubaki ni hasi kwenye account, maana yake utabakiwa na 1$. 

Kwa mfano huu Kila pip kwenye mzunguko wa bei litakuletea au litagharimu $ 0.1 ikiwa ni kwa viwango 5 vya decimali basi itakuwa ni $0.01.

Kampuni amabazo ambazo zina Kiwango kidogo cha Kuanzia na ambazo unaweza kufanya biashara ukiwa Tanzania ni hizi hapa. Tutakupa elimu taratibu mpaka ufungue Account na uanze kufanya biashara

Tembelea Tovuti kwa Kubonyeza Link


FBS:   ww.fbs.com

 

Instaforex: www,instaforex.com

 

XM: www.xmgroup.com

 

Liteforex: www.liteforex.com

 

Jinsi ya Kufungua Account Ili uanze kufanya Biashara Kwa Vitendo Mfano FBS  Broker

Nitaeleza namna ya Kujiunga na Kampuni mojawapo ya biashara za Fedha, Kampuni zipo nyingi ila ambazo zinafaa hasa watu wa kipato cha chini na cha kati ni chache. Kufungua Account ni Rahisi sana.

Hakikisha unambonyeza link hii ikupeleke moja kwa moja kwenye offer ya dolla 100. FBS market

Kampuni hii naipendekeza kwa sababu  inakianzio kidogo na faida kubwa, pia inatoa offer ya dolla.





1.     Kufungua Account ya Bonus unapewa dolla 100.

Bonyeza kitufe cha "Get Bonus" kwenye tovuti ya link www.fbs.com Utahitaji kupitia utaratibu wa usajili na upate eneo lako kibinafsi. Bonus hii ni ka wote ambao wanafungua biashara kwa mara ya kwanza.

Unaweza kujiandikisha kupitia mtandao wa kijamii au ingiza data inayohitajika kwa usajili wa akaunti mwenyewe.

Baada ya kutuma taarifa zako utapokea ujumbe kwenye email yako wa kuthibitisha usajili. Utapewa account namba na Password, zitunze vizuri.

Account ya bonus inatumika kwenye Megatrade 5 hii n platform ya biashara  ni kama browser ya kufanyia biashara.

Download aina ya platform unayohitaji kulingana na kifaa chako kuna ya computer, simu za android, Iphone n.k

Ukishaipakuwa utainstall kama program nyingine halafu utaenda kwenye File-Login utaingiza account namba na namba ya siri ulipewa, utachagua na server kwa kuwa ni demo bas utachagua FBS demo.

Tayari utakuwa umeshafungua account na upo tayari kwa ajili ya kuuza na kunua fedha na bidhaa nyingine.

2.     Kufungua Account ya Biashara.

Utahitaji kuchagua aina ya akaunti

Ukishajiunga Fbs unaweza kufungua aina tofauti ya account kwenye personal area yako. Zipo Aina mbili ya account kwa wanaoanza cent account ambayo ni kianzio dolla 1 na macro Account. Account ndogo kianzio Dolla 5. Mim nashauri kama unataka uanze biashara na upate hela uione chagua ya Macro. Lakin pai unarusiwa kuwa na aina tofafauti za account hata 10 unaweza pia kuwa na a cent kwa ajili ya kujifunzia, ukapata cent za kula.

NB; Ikiwa wewe sio mzoefu wa biashara, chagua senti au akaunti ndogo ili kufanya biashara na pesa kidogo kuanzia dolla 1 mpaka utakapojua soko.

Ikiwa tayari unayo uzoefu wa biashara ya Forex, unaweza kutaka kuchagua kiwango cha kawaida akaunti isiyo na ukomo.

Ili kujua zaidi juu ya aina za akaunti kwenye  FBS market

Lazima uweke sarafu ya akaunti yako inaweza ikawa dolla au Euro n,k.

Angalia makubaliano ya wateja wa FBS market. Hakikisha unasoma kwa uangalifu (customer agreement). Ukimaliza kusoma yote bonyeza kwamba unakubali makubaliano ya wateja na bonyeza kitufe cha "Fungua akaunti".

  Hongera! Usajili wako umekamilika. Mfumo umekutengenezea nywila/namba ya siri ya muda mfupi. Tunapendekeza Sana ubadilishe na ujenge nywila yako mwenyewe.

 

Andika nywila mpya na bonyeza "Hifadhi nenosiri". Utaona habari ya akaunti yako. Hakikisha uhifadhi nywila zako kwa uangalifu na uzihifadhi mahali salama.

 

Kumbuka kuwa utahitaji kuingiza nambari yako ya akaunti, nenosiri la biashara na seva ya biashara kwa MetaTrader 4 kuanza biashara.

Kumbuka Account ya Bishara inatumia Metatrade 4 kama platform hakikisha unaipakuwa bure kwenye www.fbs.com

Angalia barua pepe yako. Kutakuwa na barua pepe ya usajili. Fuata kiunga katika barua hii ili uhakikishe anwani yako ya barua pepe na umalize usajili.

 

Ili kuweza kutoa pesa kutoka kwa akaunti yako, unahitaji kuthibitisha wasifu wako, hii ni pamoja na kupiga picha kitambulisho na kutuma kumbuka biashara ya fedha inasimamiwa na bank hivyo ni kama unafungua account bank.

Kumbuka kwamba kwa kuwa unayo eneo lako kibinafsi kwa FBS market, utaweza kufungua akaunti zaidi za biashara wakati wowote unapenda.

No comments:

Post a Comment

Forex News